18 Septemba 2021 - 11:56
Kiongozi Muadhamu awapongeza wanamichezo waliotwaa medali katika michezo ya Paralympic na Olimpiki ya Tokyo

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amekutana na wanamichezo waliotwaa medali katika mashindano ya Paralympic na Olimpiki ya Tokto Japan ambapo amewapongeza kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, ujumbe muhimu zaidi wa ushindi wa wanamichezo wanaoliletea fakhari taifa lao katika mashindano ya kimataifa ni kufanya mambo ambayo kidhahiri yanaonekana haiwezekani kuyafanya, na kufikisha ujumbe wa kusimama kidete, matumaini na nishati kwa jamii na vijana.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria na kutoa mifano ya mabingwa na watwaa medali katika michezo ya dunia kwa njia isiyo salama na sahihi na kubainisha kwamba, dhulma ya marefa, rushwa na mambo ya kisiasa, kutumia dawa za kuongeza nguvu  ambazo zimepigwa marufuku, kuchukua medali kwa kuuza nchi na mwanamichezo kujiuza ni mifano ya wazi ya ubingwa usio salama.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa, dhihirisho la thamni za kiutu, kidini na kimaanawi sambamba na ubingwa michezoni ni jambo lenye thamani mno.

Kiongozi Muadhamu ameashiria mashindano ya michezo ya Olimpiki na Paralympic na kusema kuwa, wanawake wanamichezo wa Kiirani wamethibitisha katika michezo hiyo kwamba, vazi la hijabu siyo kizuizi cha kung'ara michezoni kama ambavyo wamethibitisha hilo katika medani nyingine kama za kisiasa, kielimu na uongozi.

Ayatullah Khamenei amesema, kutotambuliwa na kususiwa utawala ghasibu wa Israel katika michezo ni jambo muhimu sana na kueleza kwamba, utawala unaomwaga damu, unaouawa watoto na haramu wa Israel unafanya juhudi za kujipatia uhalali kupitia medani za kimataifa za michezo na mabeberu wa dunia nao wamekuwa wakiusaidiia utawala huo dhalimu, hata hivyo maafisa wa michezo na wanamichezo hawapaswi kuwa na kiguguymizi cha aina yoyote katika katika uwanja huu.

342/